Mastaa wa Kiume na Muonekano Mpya wa Rangi za Nywele Kichwani
Inaweza kuwa ni fashion mpya iliyoingia mjini kwa sasa wasanii wengi wa bongo wameanza ku-trend nayo sasa, ni upakaji wa rangi nywele.Sio mbaya kubadilisha muonekano wako hasa kwa watu maarufu ili watu wasiweze kukuzoea na muonekano ule ule kila siku lakini pia katika upakaji wa rangi hizo inabidi pia kuzingatia sana rangi yako binafsi ili uweze kutokea.
Hivi karibuni kumezuka wasanii kadhaa wa kiume wameanza ku-trend na stykle hii ya nywele kama:
.Huu ni muonekano mpya kwa Alikiba alioamua kutoka nao hivi karibuni.
BEN POL
Wengi walizoea kuona watu wakipaka rangi ya brown. lakini Ben Pol alikuja na muonekano tofauti wa rangi ya kijani kichwani mwake ambayo pia ilimfanya aonekane poa inawa mara ya kwanza wengi walimsema.
Harmonize.
Harmonize aliamua kutoka na muonekano wa kuweka breach katika nywele zake kica kizima ingawa ilizoeleka kuwa wanaume wamezoea kuweka katikati.
LAVALAVA.
Muonekano huu wa Lavalava unataka kufanana kidogo na ule wa alikiba , ambapo juzi baada ya Alikiba kuachia picha zake watu walianza kuzua gumzo kuwa kuna aliyemuig mwenzie.
OMMY DIMPOZ
Ommy Dimpoz ni moja ya wasanii wanaojali sana muonekano wao wa nje hasa katika mavazi na kila kitu kinachomfanya aonekane nadhifu na mwenye kuvutia, yeye pia alitoka na style mpya ya nywele juzi, akiwa ameweka breach.