Rayvanny Awavuta Jason Derulo na French Montana Kwenye Bongo Fleva
Msanii maarufu wa Bongo fleva kutoka label maarufu Bongo WCB, Rayvanny amezidi kudhihirisha uwezo wake baada ya jana kuachia ngoma yake inayoitwa ‘Tip Toe remix’ aliyoshirikishwa na Jason Derulo huku ndani yake akiwepo French Montana.
Jason Derulo ni msanii maarufu sana nchini Marekani lakini hivyo hivyo rapa maarufu French Montana mwenye Makazi yake nchini Marekani lakini mwenye asili ya Africa kutoka katika nchi ya Morocco.
Ngoma ya Jason Derulo ya ‘Tip Toe’ ni moja kati ya ngoma zake ambayo imefanya vizuri na kufikisha jumla ya watazamaji milioni 66 katika mtandao wa YouTube baada ya kuona mafanikio hayo ndipo alipoamua kutoa ‘Remix’ yake ambayo ndio hiyo aliyomshirikisha Rayvanny na French Montana.
Msanii huyo mkali wa wimbo wa kwetu alitangaza kutoka kwa nyimbo hiyo jana ambapo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram maneno haya:
God is good all the time, big thank you to my brother Jason Derulo for this amazing opportunity, Africa to the world, let’s go”.
Miezi michache iliyopita Rayvanny alienda nchini Marekani kwa ajili ya kufanya kazi na Jason Derulo lakini pia alisema atafanya kazi na kundi la Migos muda wowote. Hii hatua kubwa katika kuukuza mziki wetu wa Bongo fleva hakika hongera kwa Rayvanny kwa jitiahada zake.