Rushwa za Ngono Zimetawala Kwenye Tasnia ya Muziki – Witnesz
Msanii mkongwe wa rap Bongo, Witnesz au maarufu kama kibonge mwepesi ameibuka na kusema kuwa kama msanii wa miaka zaidi ya ishiririni katika tasnia hii ya Bongo fleva ameona jinsi rushwa ya ngono inavyotawala.
Siku chache zilizopita Witnesz alishangaza mashabiki zake baada ya kutoa povu kali akiwaelekezea wadau waliopo kwenye tasnia ya muziki kama Madj, watangazaji na waandaji wa muziki kutoka katika media mbali mbali akiwatuhumu kwa kuwaomba wasanii wengi wa kike rushwa ya ngono.
Imekuwa kawaida kwa wasanii wa kike kulalamika na kukata tamaa ya kufanya muziki kwa kile kinachodaiwa kuwa wanachoshwa na kuombwa rushwa ya ngono na watu mbali mbali wenye wadhfa fulani ambao wanaweza kuwa na mchango fulani kwao.
Baada ya kutoa povu hilo mtandaoni Witnesz alifanya interview na Dizzim Online ambapo alifunguka na kusema kuwa anachoshwa sana na rushwa za ngono zinazoendelea nchini ambazo zinaangaliwa zaidi kuliko kipaji cha msanii.
Nimeamua kuandika vile kutokana na rushwa mbali mbali zinazoendelea kwenye media tofauti tofauti kutoka kwa maproducer na madj vitendo ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda mrefu sasa tangu naanza mziki miaka 20 sasa ambapo nimekuwa nikivikwepa na kupingana navyo na mimi siwezi kutoka na mtu kama kigogo au viongozi wa serikalini au mtu yoyote mwenye wadhfa wake kwa maana kwamba mimi sitoki na mtu ili nipate kitu fulani kwa sababu ninajua kitu nilivhonacho kina thamani kubwa sana ambapo ninajua kwamba endapo watu wataamua kukithamini basi nitafika mbali zaidi”.
Suala la wanawake wengi kwenye tasnia ya burudani kutakwa kingono ili wapate nafasi ya kusikika sio jambo geni hapa Tanzania limekuwa likiendelea kwa miaka mingi lakini inasikitisha kwamba hakuna hatua zozote zinazochukuliwa ili wanawake wapate nafasi sawa na wanaume.