Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na wasanii kutoka Kenya watuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi 32 Arusha
Wakenya wametumama salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva walifariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Wanafunzi na walimu hao walikuwa wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta and wasanii kadhaa wametumama salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi na walimu hao.
Uhuru Kenyatta – Rais wa Kenya
Rais Kenyatta alituma pole kwa Rais John Magufuli alipokuwa akifanya kampeni zake, aliomba watu wasimame kwa dakika moja kuomboleza wanafunzi walioaga.
Mzazi Willy Tuva – Radio presenter radio Citizen
Tunaungana na ndugu na dada zetu wa Tanzania kwa Msiba uliowasibu Jumamosi kwenye ajali iliyotokea Arusha na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wao .
Mola wape nguvu wazazi, ndugu, dada, jamaa, marafiki na Watanzania wote na tuwaombee waliotuacha .
Inauma sana. Inatia majonzi sana. Tanzania hamko peke yenu, tuko pamoja wakati huu mgumu .
#TanzaniaTukoPamoja
Bahati – mwimbaji wa nyimbo za Injili
REST IN PEACE ? Just to send my condolences to Our Neighbour’s Tanzania Wamewapoteza Watoto 32 Wa Primary School kwa ajali mbaya ya Gari la Shule huko ARUSHA… We pray for Strength kwa Family zote Waliowapoteza Wapendwa. Mungu awalaze Mahali Pema!
Nyota Ndogo – mwimbaji
Mimi sina raha kabisa yani hata sioni nikiposti kitu chengine MUNGU wangu waeke pema peponi.wazazi wanalia mpaka nami nalia yani mpaka uzazi unaniiuma.watanzania poleni sana
Nameless – mwimbaji
My condolences to my brothers and sisters in Tanzania for the loss. Mola na awalaze pema watoto wetu.
#TutaonanaBaadaye
Mercy Masika – mwimbaji wa nyimbo za Injili
The loss of a child can never be replaced but our hope is in the knowledge of the one who holds our lives. Poleni sana Tanzania. Mungu anayajua haya na awape amani kwa hiki kipindi kigumu kwa wazazi marafiki na nchi yote .
Pole zetu ziwafikie , Mungu ana mpango mzuri na ni salama kwetu sababu yu hai . Amani . Arusha st vincent #MunguMfarijiWetu #RIP WATOTO WA TANZANIA.