Nikki Wa Pili Amewatolea Uvivu Watu Wanaotoa Msaada na Kamera Nyuma
Mwanamuziki wa hip hop ya Bongo fleva kutoka katika kundi la Weusi Nikki wa pili amewatolea povu kali watu wanaodai ni wasamaria wema ambao wanaenda kutoa misaada lakini wanabebea makamera ya kuwarekodi.
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kwenda kwenye maeneo mbali mbali ambamo inajulikana wanaishi watu fulani wenye maisha magumu inaweza ikawa kituo cha watoto yatima ama hata vituo vya kuishi wazee na kutoa chochote alicho nacho lakini pia ni desturi kwa watu wengi kuita waandishi wa habari.
Wasanii wengi kwenye jamii yetu hawaoni shida kuanika mambo mema waliyofanya katika jamii ni jambo zuri ndiyo lakini sio lazima ujionyeshee kweli umetoa kama kweli ulitoa kwa moyo mmoja hutahitaji kila mtu ajue ingawa huo ni mtazamo wangu tu binafsi.
Lakini inaelekea Nikki wa pili ana mtazamo kama wangu ambapo amewapa makavu watu wote ambao hawaridhiki na kutoa msaada tu lakini watataka waanike kila kona ili waonekane na kila mtu kwaiyo inakuwa ngumu kumtambua yupi ana nia gani ya kweli au yupi ana nia ya uongo:
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo:
Ukitoka na marafiki au familia au wafanyakazi wenzako mkaenda kutoa msaada kwa wenye uhitaji mkifanya nyie na wao mnakuwa mmefanya kazi ya Mungu , maana alisema ukitoa sadaka na mkono wa kushoto mkono wa kulia usijue, lakini ukienda kutoa msaada umembatana na makamera kuandaa mapicha na mavideo kusambaza mtandaoni na kwingineko utakuwa umeenda kufanya kazi ya shetani…..kuwatumia watu wenye shida kujenga jina au brand au kutafuta ushawishi au kifaa cha kufanyia propaganda…saidia kama habari zitasambaa acha zisambae zenyewe ni maoni yangu lakini naweza nisiwe sawa pia”.