Mama Diamond: Mtoto Wa Hamisa ni Mjukuu Wangu Pia
Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mama Diamond au Bi. Sandra amefunguka kwa mara ya kwanza na kukiri kuwa mtoto wa Hamisa aliyezaa na Diamond pia ni mjukuu wake.
Mwaka jana mwishoni Diamond alizua kizaazaa cha mwaka baada ya kuenda redioni na kukiri kuwa amezaa na Hamisa ambaye pia alikiri kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi kwa miaka zaidi ya tisa huku siku zote akiwa msichana wake wa pembeni wakati yupo kwenye mahusiano na mpenzi wake Zari pia aliendelea kuchepuka naye.
Lakini hata baada ya sakata hilo Zari alimsamehe baba watoto wake na wakaendelea na mahusiano yao na hapo ndipo familia ya Diamond ilipoongeza ukaribu na Zari na kumtupia mbali Hamisa na mtoto wake.
Kwa muda mrefu kumekuwa na maswali mengi juu ya sababu inayopelekea mpaka familia ya Diamond kutoweka ukaribu na mtoto wa Hamisa anayeitwa Prince Dully au Dylan kama ilivyokuwa kwa watoto wengine wa Diamond Princess Tiffah na Prince Nillan aliozaa na mpenzi wake Zari.
Lakini hivi karibuni Diamond karudi tena kwenye headlines za mitandaoni huku akiwa na skendo mpya tofauti tofauti huku safari hii ikionekana Zari ameshindwa kuzivumilia kwani aliwaunfollow familia nzima ya Diamond akiwemo shoga yake namba moja Mama Diamond.
Baada ya sakata hilo na Zari hatimaye Mama Diamond amekiri kuwa Dylan mtoto wa Hamisa naye ni mjukuu wake hii ilitokea kwenye Instagram aliporusha picha ya mjukuu wake Nillan kuna shabiki akamuuliza “Uwe unamposti hata Dylan kwani naye si mjukuu wake?”. Baada ya kubandikwa swali hilo Mama Diamond akamjibu “Usijali ntamposti yule ni mjukuu wangu hivyo lazima nyamposti tu”.