“Maisha Yangu Yamebadilika” -Wastara
Muiguzaji wa Bongo movie Wastara Juma au maarufu kwa jina lake la usanii kama Wastara Sajuki amefunguka na kudai kuwa maisha yake yamebadilika tangu alipopata ajali kwa mara ya kwanza.
Wastara alipata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita ambapo alikuwa na marehemu mume wake Sajuki ambao kwa kipindi hicho walikuwa hawajaoana lakini Sajuki na Wastara walipata umaarufu zaidi na kusisimua watu wengi baada ya Sajuki kumuoa pamoja na kilema alichopata kwenye ajali.
Wiki mbili hizi Wastara amekuwa akishika headlines za mitandao ya kijamii baada ya kuomba msaada kwa watanzania wampe pesa ambayo itaenda kutumika kama ya matibabu kutokana na kuumwa mguu wake aliokatwa ambao umekuwa ukimsumbua.
Habari zilikuja kuenea mtandaoni kuwa Wastara ni tapeli na hutumia pesa kama hizo za michango kwa ajili ya matumizi yake binafsi kama kufanya biashara lakini Wastara alikana tuhuma hizo na kusema mara ya mwisho alienda kutibiwa India na alikuwa risiti za matibabu yake.
Wastara pia amefunguka kuwa tangu apate ajali maisha yake yamebadilika kwa ujumla hivyo amekuwa akisaidiwa na marafiki zake ndugu pamoja na majirani. Wastara aliendelea kufunguka:
Natamani kuwa na foundation yangu na kituo cha watoto yatima kwa sababu tangu nilipopata ajali maisha yangu yamekuwa ya kusaidiwa tu kwa asilimia kubwa japo kuwa ni msanii na nina jina lakini vitu vingi nimekuwa nikifanya kwa kusaidiwa na mimi natamani siku moja nije kusaidia watu”.
Hivi sasa Wastara amesafiri kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu lakini pia amesisitiza kuwa hata akirudi toka kwenye matibabu hafikirii kuacha kufanya sanaa.