Mange Kimambi Apewa Siku Kadhaa Za Kuishi na Sheikh Mkuu

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni mwanadada Mange Kimambi amejikuta ndani ya vita kali na sheikh Mkuu wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa Salim baada ya kumpa Mange siku kadhaa za kuishi duniani.

Sakata hilo lilianza siku chache zilizopita baada ya picha ya Sheikh huyo kusambaa mtandaoni iliyomuonyesha kama amekaa na mgombea CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia na wanachama wengine wa CCM na habari kusambaa mtandaoni kuwa alikuwa ametoka kuwapigia kampeni.

download latest music    

Baada ya picha huyo kusambaa Mange alimtolea uvivu na kumsema kuwa ni mnafki kwani ni siku chache zilizopita sheikh huyo alikuwa ametoka kuwasema Maaskofu waliokuwa wanaongelea siasa kwenye nyumba za Ibada yaani wanachanganya siasa na dini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika maneno haya:

Sio huyu sheikh majuzi aliwasema maaskofu waliomsema Raisi Magufuli kanisani na kusema wasichanganye dini na siasa yeye hapo anachanganya maharage na mahindi au? hana hata haya…haki wakina nabii Tito wapo wa dizaini nyingi”.

Baada ya maneno hayo aliyoandika Mange na maneno mengine kusambaa Sheikh Alhad aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumtolea povu zito Mange. Sheikh Alhadi ameiongelea picha hiyo iliyosambaa mtandaoni na kusema picha hiyo ilipigwa Kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mtandaoni na kusema alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali ya raisi Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kusema Wema anautumia ulimi wake na mikono yake kutukana na kudhulumu watu na kuharibu heshima zao.

Sheikh huyo amesisitiza kuwa huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange Kimambi na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yoyote kwa ulimi wake na mikono yake kwa sababu amejihalalisha mwenyewe maangamizi kwa mikono yake amesema atamshtaki kwenye mahakama ya mbinguni.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.