Gigy Money Aponda Utaratibu Wa BASATA Kwa Video Vixens
Msanii wa muziki wa bongo ambae pia video vixen katika video za wasanii mbalimbali Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuongelea utaratibu wa Basata wa kuwaambia video vixen kutaka kujitambulisha huku wakichagua kwa baaadhi ya watu na kuwaacha baadhi yao.
Akiongea na xxl ya Clouds Fm, Gigy Money amesema kuwa anashangaa jinsi basata wanavyomtaka yeye kuisajili wakati kuwa watu wanaofanya kazi kama yake wengi na hawajaambiwa kufanya hivyo, kwanini masharti hayo anapewa yeye na wanzie wachache.
waliniambia nifanye hivyo lakini sasa Hamisa Mobeto anafanya nini, Tunda anafanya nini,officialnai anafanya nini au unataka kuniambia kuwa mavideo vixen wote wanajulikana basata kasoro mimi tu au ni kwa sababu walishaona gigy anapata chochote kitu.
Basata wataanzanje kujali utamaduni wa msanii kama hawajali ugali wake,haujui hata mfuko wake, wewe unaniona mimi nimekaa navaa napendeza unajua napoteza shingapi?
Malamiko ya Gigy Money yanakuja baada ya kutakwa kufika ofisi za basata kwa ajili ya kujiandikisha na kazi yake ya kutokea katika video za wasanii wengne.lakini pia hili ni agizo lililotolewa na Mh. rais baada ya kuona wasanii wengi hasa wa kike wamekuwa wakivaa na kuchapisha picha na video zinazowaacha uchi.
Naibu Waziri alianza kufanya utekelezaji kwa kuwafungua baadhi ya wasani na kuwambia wengine kuchukua funzo kutoka hapo.Hata hivyo Gigy Money aliamuliwa kufanya usajili wa kazi zake mara moja na kuacha kuchapisha picha za uchi katika mitandao ya kijamii.
Kwa sasa Gigy Money anatamba na kibao kipya cha mimina baada ya kufanya vizuri na kile cha papa.