Kinje Akana Mahusiano na Tunda Adai Wao ni Marafiki Waliozoeana Tu
Mfanyabiashara maarufu Bongo Kinjekitile ‘Kinje’ ambaye pia ni mtoto wa mwanasiasa maarufu Bongo Kingunge Ngombalemwiru, amefunguka kuhusu skendo inayomzunguka kwa hivi sasa na mrembo Tunda.
Siku ya jana video zenye utata zilizomwonyesha mrembo Tunda na Kinje wakiwa wanakula denda na kula bata katika maeneo mbali mbali ya starehe jambo lililoashiria kuwa wawili hao ni wapenzi labda.
Baada ya video hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku ikiwa bado haijajulikana ni nani hasa aliyesambaza video hizo mpaka hivi sasa kwani kuna taarifa zilizodai kuwa Tunda ndiye aliyesambaza video zile kwa sababu yeye ndiye alikuwa anazichukua.
Tangu video hizo zitokee kuonekana hadharani siku ya Jana, Kinje amefunguka kuhusu video zile na amedai kuwa yeye na Tunda ni marafiki wazuri tu huku akidai kupiga vile madenda ni marafiki wawili waliozoeana.
Kinje amefunguka hayo kwenye mahojiano maalumu aliyofanya na Global TV ambapo pia amefunguka mengine zaidi:
Tunda ni rafiki yangu wa siku nyingi lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi wala uhusiano mwingine wowote zaidi ya urafiki na kusema ukweli zile video zilizosambaa sijapenda na wala sijajisikia vizuri kwa sababu mimi nina mke wangu nampenda sana naipenda familia yangu sana ila mambo kama hayo saa nyingine yanaweza kutokea katika maisha ya siku hizi labda mmekutana kwenye ulevi labda Bahati mbaya vitu vikatokea kwaiyo hata mimi hili linaniumiza sababu sipendi mke wangu aumie nampenda Sana”.
Kinje ambaye ana mke na watoto wawili amekiri kujutia kitendo kile cha kuvuja kwa video zile mtandaoni na kumuomba radhi mkewe na familia yake kwa ujumla.