Shamsa Ford Akatazwa Kutumia Mitandao ya Kijamii na Mumewe.

Msanii wa bongo movie Shamsa Ford ambae amolewaa miaka miwili iliyopita, amefunguka na kuthibitisha kuwa mume wake alimwambai aache kutumia mtandao wa kijamii hasa instagram ili kuepusha shari na matusi kutoka kwa mashabiki.Shamsa Ford ambae kwa sasa amekua haonekani sana katika mitandao ya kijamii  huku sababu ikisemekana kuwa sababu ni kukatazwa na mume wake chid mapenzi.

Mtu wa karibu na Shamsa Ford alisema kuwa shamsa alikatazwa kutumia mitandoa hiyo kwa sababu alikuwa akitumia muda mwingi katika mtandao wa instagram na kuweka poicha na hata muda mwingine alikuwa akiambulia matusi kutoka kwa mashabiki kitu ambacho kimekuwa  kikimkera sana mume wake na kumfanya amkataza kuweka picha  na kutumia mtandoa huo.

download latest music    

Kampuni ya habari ya GPL,liliamua kumtafuta Shamsa Ford ili aweze kusema juu ya hilo ndipo nae alipokiri kuwa ni kweli mume wake alimwambaiaache kutumia mtandao huu kwa muda mpaka pale atakapomruhusu tena “kwa sasa naishi kwa amani sana, mana nimepumzika na matusiya kwenye mitandao sitaoni tena.sijui mume wangu aliona nini mpaka aliamua kuniambia  mpaka atakaponiruhusu kurudi tena.”

Shamsa Ford na chid mapenzi ni moja ya couple ya watu maarufu walioweza kufunga ndoa na kudumu bila kuwa na skendo wala maneno ya hapa na pale kuhusu ndoa yao, ilhali inafika muda mpaka Shamsa anatumia muda wake kuwashauri wanawake wengien kuingiakatika ndoa na jinsi ya kuishi na mume vizuri.

Madhaifu mengi ya wasanii yamekuwa yakionekana kupitia mitandoa na wamekuwa wakikumbana na matusi mengi katika mitandao hiyo.Muda mwingine kwa kujua au kutokujua mashabki hujikuta wakimu-attack msanii na kumtukana bila kujua sababu ya vitu vinavyotokea.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.