Dully Sykes Alalamika Kutopewa Heshima Kwenye Mziki
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Prince Dully Sykes amemwaga povu zito na kudai kuwa hapewi heshima anayostahili katika mziki huu Bongo fleva.
Dully Sykes ni mmoja kati ya wasanii wachache walioanzisha Bongo fleva miaka hiyo ya nyuma na ukiambiwa utaje malegend wa mziki wa Bongo huwezi kumuacha Dully Sykes amekuwa kwenye gemu tangu miaka ya 90 mpaka leo hii bado anatoa nyimbo kama ‘Bombadier’ na bado anakimbiza.
Kwenye interview aliyofanya na Clouds TV Dully Sykes amesema anashangaa ni kwa nini mpaka leo bado hapewi heshima yake kama muanzilishi wa Bongo fleva ilihali watu wote wanajua wazi mchango wake ulivyo mkubwa:
Wadau pia wa muziki huu wananisahau sana kama juzi kuna sehemu niliona watu maarufu mia moja waliofanya mambo makubwa Tanzania nikaangali angalia jina langu pale lakini likawa halipo kusema ukweli nilishangaa sana wanasahau kwamba mimi ndio nilishwawishi mpaka huu mziki wa kuimba ukaingia Tanzania mimi nasahaulika sana unajua lakini najua siku nikifa watanikumbuka unajua wengine wananihofia na ndio maana hawataki kunipa nafasi unajua kwa muziki wangu mimi nilitakiwa niwe mbali sana”.