“Sijagombana na Q- chief”- Bushoke

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Bushoke Ruta amefunguka na kukana kata kata kuwa ana bifu na msanii mwenzake mkongwe Q- chillah.

Bushoke alipata umaarufu maka ya nyuma kwa nyimbo zake zilizofanya vizuri kama ”Usiende’ na ‘Mume bwege’ na nyinginezo.

download latest music    

Lakini baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kwamba wasanii hao wakongwe Bushoke na Q- chillah wamekuwa panya na paka yaani hawapatani hata kidogo licha ya kuwa marafiki hapo awali na hata kurekodi nyimbo katika studio hiyo lakini unaambiwa nyimbo hizo zipo studio mpaka Leo sababu ya ugomvi wao.

Project ambazo walikuwa wanafanya Bushoke na Q-chillah zinashindwa kutoka hadi leo jambo lililopelekea Bushoke kuendelea mbele na kutoa nyimbo yake mwenyewe inayoitwa ‘Ngoma ya ukae’.

Kwenye interview na Enews Bushoke amekana tuhuma hizo na kufunguka yafuatayo:

Mimi na Q- chief tupo freshi mbona watu mara nyingi tu wanatuona tukiwa pamoja lakini mimi na yeye ni binadamu kwaiyo tuna utofauti kwani hata mapacha wenyewe wanakuwaga tofauti kwaiyo saa nyingine tunaweza tukatofautiana lakini hatujawahi kutofautiana kiviile lakini nashukuru Mungu tupo karibu sana yaani kwa kifupi Mimi Bushoke sijagombana na Q- chief”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.