Victoria Kimani has begged controversial blogger Nyakundi to end the beef with singer Akothee and focus on more productive things.
On Instagram, the singer, posted a long letter written in Swahili confessing that she didn’t know who Nyakundi was until the beef started.
Akothee’s beef with the blogger started after he warned Kimani to stay away from her. Since then, the two have been exchanging insults on social media.
“Wewe Victoria Kimani! Rudia Victor Wanyama. No need to waste your youth listening to sterile advise from a spent cartridge like Akothee. Ako na watoto kama 8, and you’re still child-less. Are you barren? Acha kutupwa na huyu shosh. Pata watoto wa Wanyama. Saa hii Nairobi nobody wants to date nyinyi madame wa kujifanya mko na standards. So jipange haraka before it’s too late.” wrote Nyakundi.
Letter
In her letter, Kimani said that she doesn’t depend on men and everything she has is through handwork hence Nyakundi shouldn’t bash her.
Here’s the letter:
Nitakua mwanamke wa aina gani kama kama sita ongea mambo yanayo tuumiza sisi kisaikolojia,kiroho na kimwili.Mtazamo wa jamii yetu kwa wanawake unahitaji kubadilika.
Kuanzia wauguzi wakike, wafanyi kazi wa nyumbani, waalimu, wafanyi biashara, wanasiasa, waburudishaji, wamiliki wa biashara, matajiri wanawake, maskini wanawake, wamama, madada.. watoto wakike, na hata mtoto wa kike akiwa tumboni mwa mamake…..
Kulingana na watu wachache wenye akili finyu, wanawake wote wako sawa!!
Mbona usinihukumu kwa matunda ya kazi yangu, au kwa mienendo ninayo-ionyesha katika Maisha ya kila siku? Mbona usinihukumi kwa hilo badala ya kunihukumu kwa maovu??
Hata mwenyezi mungu, ambaye mwanawe Yesu Christo, aliwaambia wanaume waliotaka kumtupia yule mwanamke Malaya mawe , ya kwamba; “asiye na dhambi, miongoni mwao, awe wa kwanza kutupa jiwe!
Athari za kutowaheshimu, wanawake tunaowajua, na tusiowajua, ni kwamba tunaifundisha jamii, nama ya kuwachukulia dada zaka, na mamako!
Sitatukana family yako, wala watu unaowapenda, kwa sababu, nina uhakika unafahamu uchungu wake!
Je, unafahamu kwamba, mimi ni mtoto wa mtu, dadake mtu, na kama kioo cha jamii, kuna wanawake wengi, ambao, wananiangalia kama kielelezo kwao?
Natumia muziki wangu kuhamasisha mabadiliko katika kizazi changu na kizazi kinachokuja.
Mashairi yangu, yanawapa wanawake motisha, na naongelea chnagamoto tunazopitia Maisha yetu kama wanawake.
Dhana uliyoileta kwetu, ni za kiubaguzi kwa wanawake, ni za kukera, na kutia kichefu chefu, na zinavunja moyo.
Nimeongea katika jukwaa la umoja wa mataifa (United Nations) kuhusu umuhimu wa wanawake kua na sauti katika jamii yetu.
Na fanya kazi kwa bidi, sijawahi kuwa na sugar dady, na siwahukumu wanaofanya hivo.
DNaomba, nafunga , na naweka nguvu zangu zote katika muziki wangu, na napenda ninachokifanya.
Siko hapa kukudhalilisha, bali niko hapa kukuinua.
Cyprian Nyakundi Sikuwahi kukujua, mpaka uliponitaja mimi na mmoja wa marafiki zangu wa karibu Akothee.
Lakini nafurahi kujuana na wewe mtandaoni.
Kunijua, ni kunipenda, na pia ni kuniheshimu mimi, na juhudi zangu za kimaisha.
Namtakia kila anayesoma huu ujumbe Amani na Furaha!