Irene Uwoya apologizes after throwing money to journalists
Actress Irene Uwoya “made it rain” with money during a press briefing recently and some were not happy.
Uwoya almost caused a stampede at Hyatt Regency on Monday, July 15 after she started throwing money to journalists after a press conference.
“Tarehe 31 ni siku ya kumbukumbu kwa wasanii sisi bongo movie, haijawahi kutokea hiyo kitu itakayotikea Mlimani City itaweka historia, itakuwa ni red carpet ya funga mwaka. Kwa hiyo ndugu zetu waandishi mjipange hata kwenye kuvaa mjipange. Msituangushe sasa mje masuti nini msije kama hivi tulivyozoea,” Uwoya told reporters.
Ndugu zangu Waandishi wa Habari…mnaaibisha taaluma yenu. pic.twitter.com/YbDxqqkFhZ
— Lusajo L.M. | 1440 (@Sajjo) July 15, 2019
Sorry
The act got a lot of backlash forcing the actress to come out and apologize. In the apology, Irene said that she wasn’t after demeaning journalists or causing a fracas.
Ndugu zangu waandishi wa habari, leo katika press conference ya Swahili Inflix na ndugu zetu waandishi wa habari niliamua kutoa fedha kwa style ya kutunza.
Baadhi yenu mmekwazika kwa kitendo hicho nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, binafsi nawapenda waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu sana katika jamii.
“Sikufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa.Kama binadamu moyo wangu ulijawa na upendo na furaha iliyopitiliza ndipo niliona niweze kushiriki nanyi furaha hiyo kwa aina ile ya kuwatunza pesa,sababu mara nyingi mmekuwa watu muhimu katika kazi na mambo yote yanayohusu sanaa yetu na jamii kwa ujumla.
Na baadhi ya waandishi ambao kwa bahati mbaya waliharibu vifaa vyao wakati wa kuokota shukrani yangu hiyo(pesa) naomba mniwie radhi na mnisamehe sana na poleni sana kwa changamoto.” she said.
Adding:
“Pia kuhusu ndugu zangu waandishi kuwaomba kuvaa suti ile nilikuwa na maana nzuri ya kwamba katika utanashati wenu wa kila siku sisi tulipendelea siku ya tar 31st August katika show yetu inayoandaliwa na Swahili Infilix itakayokuja kuleta mapinduzi makubwa na ukuaji mkubwa zaidi wa filamu zetu za hapa nyumbani tunatamani kuona wote mkiwa katika uniform ambayo itawatambulisha vyema kimavazi ambayo kwa wazo letu tuliweka suti na kiukweli mtapendeza sana na zaidi ya kawaida tulivyozoeana.Nawapenda sana maana hakuna mimi bila nyinyi nathamini na kuwashukuru sana sana.Na zaidi naomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa namna moja au tofauti.
Asanteni sana.”